Uturuki imemuondoa balozi wake kutoka Vatican, baada ya Papa Francis kuyataja mauaji ya waarmenia wengi kuwa mauaji ya halaiki ya kwanza ya karne ya 20. Papa Francis alitoa matamshi hayo wakati wa Misa ya Jumapili mjini Rome, iliyoadhimisha miaka 100 tangu wakristu wa Armenia walipopambana na wanajeshi wa himaya ya Uthman. Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu, amesema matamshi ya papa yako mbali kabisa na ukweli wa kisheria na kihistoria, na kwamba yanachochea chuki dhidi ya Waislamu na Waturuki, badala ya kuleta maridhiano. Ingawa papa Francis hakutumia maneno yake mwenye kuyataja mauaji hayo kuwa ya halaiki, kwa kumnuku Papa John Paul wa pili, alibainisha msimamo wa kanisa juu ya suala hilo, amesema mchambuzi wa Vatican Marco Tosatti.
13 Aprili 2015 - 08:50
Msimbo wa Habari: 683268
Uturuki imemuondoa balozi wake kutoka Vatican, baada ya Papa Francis kuyataja mauaji ya waarmenia wengi kuwa mauaji ya halaiki ya kwanza ya karne ya 20.